Latest Updates

HALI BADO TATA KIGOMA, HAWATAKI KUSIKIA KUHUSU CHADEMA KAMA ZITTO KABWE HAYUPO


Baada ya mkutano wa Dr. Slaa Kuvunjwa  kwa fimbo  na mawe, kilichofuata  baadae  ni  mapambano  kati  ya  polisi  na  wananchi  wanaompinga Dr. Slaa .
Mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbroad Slaa uliofanyika Uwanja wa Kiganamo, Kasulu Mjini leo umevunjika baada ya polisi kupiga mabomu ya machozi wakikabiliana na vijana waliorusha mawe kupinga mkutano usiendelee.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, vijana hao wanadaiwa kuwa kati ya 20-25 ambao walirusha mawe baada ya wananchi kuwafukuza wakitaka kuwapiga wakipinga kitendo chao cha kupiga kelele ili mkutano usiendelee ndipo polisi walianza kulipua mabomu ya machozi na mkutano kuvunjika.