Kijiji cha Qunu ambako atazikwa Hayati Nelson
Mandela, kinaomboleza kifo cha shujaa aliyetoka katika kijiji hicho
Nelson Mandela. Mazingira hapa ni ya kipekee, mchanganyiko wa nyumba za kisasa na za kitamduni ambazo mfano wake ni mizinga ya Nyuki. Visima
vya maji anavyovikumbuka Mandela bila shaka hawezi kuviona sasa. Lakini
viwanja vya kijiji hiki viko chini ya majabali ambayo yeye na rafiki
zake walikesha wakichezea.
Ni viwanja hivi ambapo Madiba alijifunza kuwinda Ndege , kuchukua
asali misituni na matunda ya misitu ambayo ilikuwa inaliwa wakati huo. Alipokuwa
na umri wa miaka 5, Mandela aliandika kumbukumbu zake kuhusu safari
yake alivyopigania uhuru wa Afrika Kusini, pia alijifunza kuchunga
Ng’ombe, na kupitia kwa kazi hiyo alijifunza uhusiano uliopo kati ya
watu wa kabila la AbaTembu na Ng’ombe wao.
Alisomea
hapa Qunu, lakini kijiji alichokiacha kwa huzuni wakati alimzika babake
kimebadilika. Lakini aliporejea hapa mwaka 1990 alipokuja kutembelea
kaburi la mamake , alisema aliona umasikini mkubwa machoni mwa watu wa
Qubu, viwanja visafi alivyovikumbuka havikuwepo tena, vilikuwa vimejaa
takataka kit ambacho hakuwahi kukiona tangu alipokuwa mtoto.

Mazishi ya Mandela yamefanywa kuambatana na tamaduni za watu wa Xhosa
Mazishi ya Mandela pia yamejumuisha tamaduni za watu wa jamii ya Xhosa ambako ukoo wa Mandela wa Thembu unatoka. Bila shaka mazishi ya Mandela katika kijiji cha Qunu yatakuwa mchanganyiko wa mila na tamaduni , dini ya kikristo na pia watakaofika kutoa mazishi ya kitaifa.

Watu wa jamii ya Xhosa ambao ni moja ya kabila kubwa zaidi Afrika Kusini ikiwa na watu milioni saba wanatoka Kusini Mashariki mwa nchi katika mkoa wa Cape Mashariki. Watu wa kabila la Xhosa wanatambua mizimu ya mababu zao na wao huzungumza nayo wakati wakitaka msaada.
Wanaamini kuwa lazima mwili ujulishwe kinachofanyika kabla ya kuuzika Wanasema kuwa Madiba Lazima afahamishwe Jumapili kuwa anazikwa . Lazima jeneza lake litafungwa kwa ngozi ya Chui kwa sababu alikuwa mtoto wa mfalme wa kitamaduni. Lakini kwa sababu Madiba alikuwa Rais wa zamani , lazima pawepo bendera ya nchi. Bila shaka hii ni ishara ya heshima kwa kiongozi mheshimiwa.
Ng’ombe atachinjwa mapema alfajiri na kuliwa na watu waliofika kwa maombolezi. Na baada ya mwaka mmoja tangu kuzikwa kwa Madiba, Ng’ombe mwingine atachinjwa na kuliwa na familia ishara kuwa maombolezi yamekwisha.