West
Brom wameshinda Old Trafford msimu huu baada ya miaka 35...Everton
baada ya miaka 21 na Newcastle baada ya miaka 41...YOTE HAYA YAMETOKEA
BAADA YA FERGIE KUSTAAFU NA KUMKABIDHI MOYES TIMU.
HAYA NDIO MAONI YA MASHABIKI:
Kweli kuna tofauti kubwa sana kati ya Sir Alex Ferguson na David Moyes.
Lakini ukiangalia kwa jicho la tatu, nakubaliana na kauli ya Moyes
kwamba anahitaji kupata wachezaji wa kiwango cha dunia angalau hata
watano.
Mpaka kufikia hapa kamjaribu kila mchezaji. Zaha ni
kichekesho, sio wa kubadilisha matokeo, Januzaj bado anatakiwa aendelee
kuchezea U21 pengine kajisahau.
Wachezaji wanaonyesha kiwango duni sana, tutaendelea kuwalilia baadhi ya wachezaji kwamba hampangi fulani na fulani tutaanza na Fletcher sasa.
Moyes apewe fungu asajili wachezaji anaotaka hapo januari kisha tuje tumbebeshe lawama vizuri.
Lakini kwa wachezaji hawa wasiojituma tutaendelea kuporomoka zaidi.
Shukurani zangu ni kwa Wayne Rooney ambae amekuwa mpiganaji wakati
wote, tumuongezee wachezaji watatu au wanne wenye moyo wa upiganaji kama
yeye watatusaidia.
