Latest Updates

MR NICE ATOA SIRI ZA NDANI ZA KABULA NA LULU JOHN, soma alichosema

Na Jelard Lucas
King wa swagga za TAKEU Afrika Mashariki aliye the big boss wa Bush Band, Nice Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ amejibu mapigo kwa ‘kuwavua nguo’ waliokuwa wapenzi wake, mcheza filamu Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ na msichana wa mjini, Lulu John, Amani linakupasha.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu ya kiganjani akiwa kwenye kampeni za CCM Kahama, Shinyanga, Nice aliwachana vibaya warembo hao na kudai kuwa hajawahi kuanguka nao dhambini kama wenyewe wanavyobandika mabango jijini Dar.

Mr Nice akiwa na Jini Kabula.
Huku akiwahusisha warembo hao na skendo mbaya ya uchangudoa, Nice aliwaruka vibaya huku akidai jambo linalomkera zaidi ni kitendo cha Kabula na Lulu kujipakazia kuwa yeye ni mume wao.

Nice aliendelea kuwapaka ile mbaya wasichana hao wanajiita watoto wa mjini huku akidai kuwa hafanani na sampuli yao hata tone.

“Wamechanganyikiwa na maisha, mtu huwezi kuitwa Jini, kwanza nawashangaa sana kwasababu siwatambui, wasitake kutafuta umaarufu kupitia kwangu,” alisema Nice anayejiandaa kwenda nchini Norway katika mwaliko wa kikazi.
Lulu John.
Amani lilimtafuta Jini Kabula na kumsomea ‘eituzedi’ ya aliyotoa Nice ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Hawezi kututukana sisi wakati tumemfuga hapa mjini, hana lolote sisi hatuwezi kujipendekeza kwake, suala la uchangudoa, hatujawahi kujihusisha na ufuska huo.”