Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 19, alipewa
kifungo cha nje cha miezi sita kwa kile mahakama ilisema ni kutoa
taarifa zisizokweli.
Atalazimika kukaa nyumbani kwake bila kutoka nje kwa miezi sita.
Mmoja wa waandishi wa habari, aliyemhoji
mwanamke huyo naye alipewa kifungo cha nje cha mwaka mmoja huku mwenzake
akipokea kifungo cha miezi sita.
Waandishi hao wanafanya kazi na kituo cha redio
Shabelle ambacho serikali ilifunga matangazo yake mwezi Oktoba baada ya
polisi kuvamia ofisi zake.
