Ajali ya meli yasababisha waziri mkuu ajiuzulu cheo chake.
Baada ya ajali ya meli huko South Korea serikali ilikosolewa kwa jinsi ilivyodili na ajali hiyo. Meli hiyo ilivyozama sehemu kubwa ya abiria walikuwa ni wanafunzi na watu kama 100 hawakupatikana.
Kwenye hatua za ukoaji zilitumika meli 34 na helicopter 18 na njia nyingine lakini pia ukosoaji kwa serikali ulikuwepo. Kutokana na hilo waziri mkuu Chung Hong-won ametangaza kujiuzulu baada ya wananchi kutoridhishwa na utendaji wa serikali kwenye hili tatizo.
Chung Hong-won aliwahi kuzomewa na kurushiwa chupa za maji wakati alipotembelea waathirika wa ajali hiyo.
Posted