NI gumzo la aina yake ndani ya mji wa Kibaha mkoani Pwani ambapo mume wa mtu aliyejulikana kwa jina la Vedasto Ager (43) mefariki dunia baada ya kupata ajali ya kugongwa na gari aina ya Fuso akiwa amempakiza mke wa mtu kwenye pikipiki.
Mwili wa marehemu Vedasto Ager ukiwa kwenye jeneza tayari kwa kuagwa.
Kifo cha Vedasto kilichotokea Aprili 6, mwaka huu kimeacha maswali kibao kutokana na muda wa tukio hilo kuwa usiku wa saa saba.
Mwanamke huyo alijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwa mujibu wa chanzo kimoja, marehemu Vedasto alikuwa akifanya kazi ya kuuza tiketi kwenye mabasi yaendayo mikoani huku mwanamke huyo akifanya kazi ya kuuza chakula ambayo ni maarifu kwa jina la Mama Lishe.
Uwazi lilipata bahati ya kuzungumza na mume wa majeruhi huyo, Fautunatus Simon ambapo alisema: “Mimi nilikuwa napita, ghafla niliona ajali.
Waombolezaji. Vedasto aliingizwa mochwari lakini mke wangu alipelekwa Muhimbili.” Akizungumzia tuhuma za marehemu kuwa na uhusiano na mke wake, mume huyo alisema hata yeye amezisikia na akasema atamuuliza mkewe akipata nafuu. “Binafsi marehemu nilikuwa namfahamu sana lakini sijapata ukweli kuwa usiku ule walikuwa wanatokea wapi?” alisema.
Kamanda wa Polisi tukio hilo. “Gari lililosababisha ajali hiyo halijapatikana lakini polisi wanaendelea na upelelezi,” alisema.