Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika kijiji cha Roo,
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro, linamshikilia Yusufu Njau (32), mkazi wa kijiji cha Roo Wilayani Hai mkoani humo, kwa kosa la kuwauwa wazazi wake ‘kikatili’ kwa kuwakata na mapanga kichwani na kisha kuchoma moto nyumba waliyokuwa wanaishi wazazi hao.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Robert Boaz, Jumatatu Mei 12, 2014 kuwa mtuhumiwa huyo aliyefanya kitendo cha kinyama Mei 09, 2014 saa kumi na mbili za jioni nyumbani kwao, ambapo kupitia msako ulioendeshwa na Jeshi hilo kuanzia siku ya tukio ambapo leo (Jumatatu) saa mbili asubuhi lilimkamata akiwa nyumbani kwa kaka yake Alifa Shaibu.
Tarafa ya Masama, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wakiwa katika sala ya mazishi ya marehemu iliyofanyika Mei 10, 2014, ambapo Shahidu Njau na mkewe Minei Swai, walipokutwa na mauti baada ya kucharangwa/katwa mapanga na mtoto wao Boaz, amesema mtuhumiwa alimuua Baba yake mzazi, Shahibu Hassan (60), pamoja na Mama yake mzazi, Minae Mohamed (57), ambao waliozikwa Jumamosi, Mei 10 2014 katika makaburi ya familia kijijini hapo.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Roo, Alfani Swai, alisema mtuhumiwa huyo alitoka kutoka alipokuwa amejificha baada ya kukumbwa na njaa kali ndipo alipoenda nyumbani kwa kaka yake ‘Alifa Shaibu’ kwa nia ya kuomba chai.
Amesema mara baada ya mtuhumiwa huyo kufika kwa Kaka yake alipata simu kuwa mtuhumiwa huyo yuko katika nyumba hiyo, ndipo alipowasili na kumpeleka mtuhumiwa katika katika kituo cha Polisi Bomang’ombe. Wananchi wateta
Mara baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo wananchi wa kijiji hicho walisema kwa sasa wataishi kwa amani kijiji hapo, kutokana na kuwa na mashaka na mtuhumiwa huyo aliyekuwa akisumbua kijiji hicho kwa muda mrefu.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa hali ya usalama nchini, inaonekana kutia shaka wananchi kufuatia mfululizo wa matukio ya watu kutekwa, kuteswa hata kuuawa kwa ndugu wa familia moja wa watoto na baada ya mda watuhumiwa huripotiwa kukamatwa katika maeneo mbalimbali nchini na sheria kuelezwa inaanza kuchukua mkondo wake kwa kuanzisha upelelezi wa matukio hayo.
chanzo Fikra Pevu