Latest Updates

AUDIO YA STEVE NYERERE AKIONGELEA MSIBA WA ADAM KUAMBIANA


Mwenyekiti wa Bongo Movie Steve Nyerere amezungumza na Clouds Fm muda mfupi uliopita kuhusiana na kifo cha ghafla cha msanii mwenzao, Adam Kuambiana ambapo ameleeza kiundani chanzo cha kifo hicho na taratibu zingine za msiba.

“Mwenzetu Adam Philipo Kuambiana amefariki akiwa Location ana shoot,mimi nimepigiwa simu saa 3 asubuhi kuwa hospitali pale Mwenge niende nikahakikishe kuwa ni kweli Adam amefariki na kweli kufika pale nikamkuta Adam Kuambiana amefariki”


“Sasa hivi tumetoka Muhumbili kwenda kumsitiri mwenzetu,taarifa inasema wakati yupo location alikua analalamika tumbo linamuuma linamuuma kumfikisha hospitali ndipo umauti ukamfika”....Steve Nyerere