Latest Updates

KIFO CHA RACHEL WA BONGO MOVIES CHAMGHARIMU NISHA, CHEKI HAPA




Salma Jabu Nisha/ Tanzanian Actress

MWANADADA Salma Jabu Nisha asitisha kutoa Filamu yake mpya kesho tarehe 29/05/2014 airusha tarehe na kutarajia kuitoa tarehe 12/06/2014 kufuatia kifo cha msanii mwenzake Rechel wa Bongo Movies.


"habari mashabiki wangu wa ukweli?,nyumbani kwetu akifa baba au dada au mwanafamilia yeyote,basi kama kuna aliyetaka kuolewa harusi inaghairishwa,maisha yangu ni filamu,na filamu ni nyumba yangu ya pili,sisi kama NISHA'S FILM PRODUCTION na STEPS INTERTAINMENT tumeamua kughairisha kuitoa filamu yetu mlokuwa mkiisubiri kwa
hamu "ZENA NA BETINA" ilikuwa itoke tar.29/05/2014 sasa basi tutaisogeza mbele hadi tar.12/06/2014 kwa ajili ya kuomboleza misiba, Samahani kwa usumbufu uliojitokeza,


Munisamehe sana,tumeguswa sana,kwangu mm km Nisha kutoa filamu ni furaha,siwezi kufurahi siku tunayomzika msanii mwenzetu kipenzi Rachel yaani kesho ambayo ndio ilikuwa siku ya kutoka ZENA NA BETINA,


Nna imani kubwa kama ingekuwa mimi Filamu isingetoka kesho na hii ni zawadi yenu Rachel na Adam kuambiana,


Kutoka NISHA'S FILM PRODUCTION. .. naomba mnisamehe sana mashabiki wangu,

Ila nimetazama UTU KWANZA halafu pesa baadae. wanaoendelea kufanya promo wafanye na naomba mnisaidie kusambaza ujumbe huu. . Nawapenda sana. ZENA NA BETINA itatoka tar.12/06/2014 inshaallah siyo tar.29 tena.Cc @nishasfilmproduction @nishasfilmproduction