Latest Updates

MAKUBWA HAYA...!!!! MAMA MZAZI AMLIPUA MOTO MWANAYE... SOMA HAPA!!


Mtoto Samwel Paulo akiwa hospital baada ya kufanyiwa kitendo cha kinyama na mama yake mzazi.
Dunia haina huruma! Mtoto Samwel Paulo (13), anayesoma darasa la nne Shule ya Msingi Amani wilayani Ilala, Dar, amelazwa wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akiendelea kuuguza majeraha yaliyotokana na kile kinachodaiwa ni kulipuliwa kwa moto na mama yake mzazi aliyetajwa kwa jina la Doricus Iganga. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea nyumbani kwao maeneo ya Mombasa Gongo la Mboto, Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, saa 8:00 usiku ambapo mwandishi wa habari hii alimtembelea wodini hapo.
Alipoulizwa kisa na mkasa hadi kuwa katika hali mbaya kiasi hicho, mtoto huyo alikuwa na haya ya kusema:
“Najisikia vibaya sana kutokana na maumivu makali ya moto. Sikutegemea kama mama yangu mzazi angenifanyia hivi kwa kunituhumu kuwa nimemuibia fedha zake shilingi elfu kumi.
“Amekatisha ndoto yangu ya masomo, kwa sasa wenzangu wanajiandaa na mtihani wa muhula, mimi nipo wodini (huku akiangua kilio).
“Matukio kama haya huwa nimekuwa nikiyasikia yakifanywa kwa watoto wenzangu kutoka kwa mama wa kambo na siyo kwa mama mzazi kama ilivyotokea kwangu.