Latest Updates

MAREHEMU ADAM KUAMBIANA KUZIKWA JUMANNE KATIKA MAKABURI YA KINONDONI DAR

Mazishi ya muongozaji na msanii wa filamu Adam Kuambiana yatafanyika Jumanne (May 20) katika makaburi ya Kinondni jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na BLOG HII, mwenyekiti wa bongo movie ,Steve Nyerere amesema kuwa marehemu ataagwa Leaders Club siku hiyo hiyo kabla ya mazishi.

“Habari za mazishi ni kwamba atazikwa siku ya jumanne na tutazika katika makaburi ya Kinondoni, kuagwa ataagwa siku hiyo hiyo katika viwanja vya Leaders Club kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 9 na baada ya hapo tutaelekea makaburini,” alisema.

Pia Steve Nyerere amedai kuwa marehemu Adam Kuambiana alikuwa na matatizo ya tumbo ambayo ndo yadaiwa chanzo cha kifo chake. “Marehemu alikuwa anasumbuliwa na tumbo tu, yani alikuwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo na hivyo ilivyotokea.”