MKALI wa vichekesho Bongo, Haji Salum ‘Mboto’ ameibuka na kusema
kuwa endapo atafariki dunia mwili wake ukaagiwe katika Viwanja vya TCC
Chang’ombe na siyo Leaders kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa wasanii
wengi wanapokufa.
Akizungumza na paparazi wetu kwenye Viwanja vya Leaders wakati wa msiba wa msanii mwenzake, achel Haule ‘Recho’, Mboto alisema tayari ameshaacha wosia kwa marafiki zake kwamba siku akifariki dunia mwili wake uagiwe TCC kwani yeye nyumbani kwao ni Temeke na ndugu zake wengi wapo huko na endapo wosia huo utakiukwa jeneza lake litagoma kubebeka.
“Mimi nimeshawaambia marafiki zangu kwamba siku nikifa mwili wangu uagiwe TCC Chang’ombe kwa sababu ndiyo nyumbani kwetu, naomba wale niliowaambia walizingatie hilo wakiona linakiukwa wagome na jeneza langu ligome kubebeka,” alisema Mboto.