Latest Updates

Ni zamu ya wenye haya meno sasa, wanalalamika kukosa wapenzi na kukimbiwa


Ni kawaida kukutana na mtu mwenye meno ambayo yameharibika rangi kwa kubadilika kutoka kuwa meupe na kuwa ya kahawia huku ambapo chanzo kinatajwa kuwa aina ya maji ambayo mtu huyo amekua akinywa/akitumia kwa kipindi kirefu.

Huko Kenya sehemu inaitwa Baringo kuna wananchi wamejitokeza mbele ya kamera ya CITIZEN TV na kukiri kwamba haya meno yamewaletea balaa la kukimbiwa na wapenzi kila kukiamka.

Kwenye ripoti ambayo unaweza kutazama ripoti yenyewe kwenye video mwishoni, kuna mmoja wao anaitwa Yvonne mrembo mwenye umbo la kuvutia lakini ni mpweke licha ya kuwa na hamu ya kupata mchumba, tabasamu lachungulia tu kwa sababu anaona aibu sana kufungua mdomo zaidi, pamoja na urembo wake Wanaume wanamkimbia.

Anasema ‘kuna mtu mwingine anaweza kukuumiza na anakwambia wewe funga mdomo, hiyo meno ya brown hapana…..’


Huyu ndio Yvonne ambae ni mwalimu wa Sekondari

Angela anasema ‘Mtu unafungafunga kwanza mdomo mwingine asione lakini baadae kwenda kuangalia anasema kumbe imeoza…’
Meno mekundu yamewakosesha furaha ya uchumba ambapo Wanaume wamekua wakijiepusha na Wasichana wenye meno hayo ambapo Mwanaume mmoja amekaririwa akisema ‘unakutana na msichana mrembo ana kila kitu unachokitaka ila likija swala la kutabasamu…. yani unaamua kupotezea kabisa mpaka unaamua umuache’

Mwanaume ambae ana tatizo la meno hayo amesema kuongea usiku ndio inaweza kuwa afadhali au kama ni mchana ukiwa unaongea inabidi uweke mkono mdomoni.


Yvonne

Kiwango cha juu cha madini ya Floride kwenye maji husababisha meno kubadilika rangi na kuwa hafifu ambapo madini hayo hupatikana kwenye maji ila yakiwa ya kiwango cha juu husababisha meno kuoza.

Maji ya aina hiyo yanapatikana pia sehemu inaitwa Maji ya Chai Arusha ambapo asilimia kubwa ya wakazi wa siku nyingi kwenye eneo hilo na maeneo jirani wamekua na tatizo la meno kuoza.


Huyu jamaa ni dereva wa bodaboda anasema meno yake yanafanya mpaka abuguliwe hata kupata kazi mfano kupata kazi ya Uaskari.