Msichana mmoja aliyetajwa kwa jina la Halima aliyedaiwa kuwa ni mchumba wa mtu, hivi karibuni alipata aibu ya aina yake baada ya kukutwa amezimika barabarani.
Msichana aliyetambulika kwa jina la Halima akiwa hajitambui baada ya kulewa chakali Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Kijitonyama jijini Dar ambapo ilidaiwa kuwa, binti huyo akiwa amevalia kimini alishuka kwenye Bajaj na kwenda kwenye hoteli iliyopo maeneo hayo bila kujulikana alikotokea.
Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Stella alisema: “Huyu dada namjua, ana mchumba wake waliwahi kufika dukani kwangu kufanya ‘shopping’. Leo asubuhi alikuja hapa na kuuliza kama atapata maziwa, alikuwa amevaa kihasara, wakati tunaendelea kuongea naye, akaanza kulegea na kuanguka.
Waandishi wetu walipofika eneo la tukio walimkuta binti huyo akiwa hajitambui na alipomwagiwa maji ya baridi alizinduka na kusema; “hapa niko wapi, nimeaibika!”