Latest Updates

PICHA: STEREO AKUTANA NA DADA YAKE AMBAYE HAWAJAWAHI KUONANA TANGU WAZALIWE



Stereo akiwa na Dada yake waliyekutana kwa mara ya kwanza Tangu wazaliwe



Hivi karibuni James Joseph Masanilo a.k.a Chunda Badi B Boy Stereo, Rapper ambaye yuko chini ya label ya Unity Entertainment alikutana na ndugu yake wa damu ambaye hakuwahi kumwona tangu ndugu huyo anazaliwa zaidi ya miaka 20 iliyopita, Ndugu huyo wa Stereo ni wa kike anaitwa Bianca anaishi jijini Dar es salaam na anasoma katika chuo cha Magogoni, Alizaliwa mwaka 1991, ameshare baba mmoja na Stereo, na mzee wao alifariki mwanzoni mwa miaka ya 2000, Rapper huyo anadai kuwa walikua wanaskia tu kuwa kuna ndugu yao wa kike yuko Moshi kwani Baba yao alimwachia Usia Shangazi yake Stereo amlee mtoto huyo, Baada ya Mama mzazi wa Bianca kufariki dunia, Stereo alipata namba za binti huyo na kuamua kumtafuta juzi wakaonana na kushangaa jinsi Bianca alivyofanana na familia watu wa familia yao sana, pia anampango wa kumtambulisha Dada huyo kwa familia kwani hakuna hata mmoja anayemjua kuanzia kaka na dada zake mpaka mama yao mzazi, Stereo akamalizia kwa kusema Bianca hajui kama Stereo ni Rapper Maarufu Tanzania.
Hapo inamaanisha dingi yake Stereo alichepuka ndio akampata Bianca.