
WALIOSEMA ujana ni maji ya moto hawakukosea. Mkali wao kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ni msanii ambaye ana idadi kubwa ya msururu wa wanawake ambao ametoka nao kimapenzi ambapo, wapo wanaojulikana na wengine hawajulikani.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Leo katika makala haya tunakuletea wanawake ambao kwa nyakati tofauti walibanjuka kimapenzi na Diamond ambao kimsingi kutokana na idadi yake, anadhihirisha jina lake la Sukari ya Warembo.
Takwimu zinaonesha kuwa karibu kila mwaka jamaa anabadilisha wapenzi ambapo wanawake wamekuwa wakipokezana vijiti.
UPENDO MUSHI ‘PENDO’
Huyu ni msanii wa filamu ambaye alitokea katika Shindano la Maisha Plus. Aliwahi kukiri kwamba alishatoka kimapenzi na Diamond kabla hajawa maarufu kama alivyo sasa, hawakudumu muda mrefu.
WEMA SEPETUNi mlimbwende wa Tanzania na msanii wa filamu kwa sasa. Diamond baada ya kupata umaarufu kidogo, alikutana na Wema na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi jambo lililofanya umaarufu wake kuzidi mara dufu.
Wema na Diamond waliachana na kila mmoja akawa anaendelea na maisha yake lakini mwaka jana wawili hao walirudiana na mpaka sasa wapo pamoja.