Unaweza kuona kama bado drama zinaendelea lakin ni kama movie imefika mwisho, kwani wale wakali wawili waliotengeneza headline hapa mjini kwa social media wamepatana, Kajala Masanja na Wema sepetu. Hii imetokea jana kwenye msiba wa director na aliyekuwa mzazi mwenzie Monalisa.
Juzi kwenye msiba wa Rechal pale makaburini kulikuwa na makundi huku Kajala akiwa na sare tofauti na as well Wema alivaa sare ya peke yake lakini hii inaweza kuwa tofauti katika msiba wa Tyson kwani wawili hao walipatanishwa wakiwa msibani hapo na kuamua kuyamaliza kwani hakuna mfano mzuri katika maisha ya mwanadamu kama kifo, kwani kinamkumbisha kila mmoja wetu kuishi vema na kwamba kesho tutaondoka .
Wawili hao walitofautiana kwa sababu wanazojua wao wawili na Instagram kuchochea ugomvi na kuwasemea vitu ambavyo hata wawili hao hawajaongea mwisho wa siku Wema na Kajala ikawa wanapishana kama train za Umeme au bus ya mwendo kasi but final wamepatana na kupeana mikono .lets hope wamesafisha mioyo yao na waishi kama zamani.