KIFO CHA WANAFUNZI CHUO KIKUU UDSM
Marehemu Sekabenga Pius Mwakimenya enzi za uhai wake
familia ya denti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, marehemu Sekabenga Pius Mwakimenya (21) kilichotokea hivi karibuni na kugubikwa na utata, imeanika ukweli kuhusiana na tukio hilo.Akizungumza na Uwazi, mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, baba mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Mwigune alisema, taarifa waliyopewa na daktari aliyemfanyia uchunguzi inamaliza utata na minong’ono yote inayoendelea chuoni.
Alisema, kwa mujibu wa ripoti hiyo, kifo cha Sekabenga kimetokana na mzunguko wa damu katika mishipa kutokuwa sawa, jambo lililosababisha ajisikie vibaya na hatimaye kufariki dunia.
Mwili wa marehemu Sekabenga Pius Mwakimenya ukiwa kwenye jeneza.
“Daktari amesema kwamba mishipa ya damu haikuwa ikifanya kazi vizuri hali iliyomsababishia ajisikie kuchoka kwa sababu damu haikuwa ikifika sehemu zote za mwili wa marehemu,” alisema Mwigune
Posted