Latest Updates

MAMA KANUMBA AMCHIMBA MKWARA MDOGO WAKE KANUMBA



MAMA wa Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amemchimba mkwara mzito mdogo wa marehemu, Seth Bosco baada ya kuona amefanya kosa na kuamua kumtishia kuwa atamfuta kwenye Kampuni ya Kanumba The Great.
Mama wa Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa
Mama huyo pasipo kuweka wazi moja kwa moja tatizo, alisema kuwa kuna kosa kubwa Seth alilifanya na

alishindwa kulivumilia hivyo kumuonya kuwa atamuondoa kwenye kampuni.“Ni juzi tu amefika nyumbani kwangu kuniomba msamaha nimemsamehe kama mtoto ingawa kwenye kampuni hatashiriki kwa sasa kwani ameanza kazi zake nyingine,” alisema.