"Kwenye mahusiano ya kimapenzi ni vizuri uzito wa mahusiano uwe pande zote mbili, mapenzi huwa matamu zaidi iwapo umpendae naye anakupenda kwa kiwango umpendacho wewe, na si vinginevyo maana tofauti na hapo mapenzi huwa kama kero au mzigo na hisia hukupelekea kujiumiza moyo na kujiharibu kisaikolojia".
Wewe ni mtu mzuri na unampenda sana msichana wako, kiasi kwamba unamkubali sana mpaka unampa dunia yako kumuonyesha unavyomjari, ndani ya muda mrefu mliopo kwenye uhusiano umeshajitoa kwa mengi, kimuda na hata kifedha, unamchukua kutoka kazini kila siku ndani ya juma ili tu asije kuchosha miguu yake mizuri na laini.
Unamsaidia kwa kila jambo analohitaji na umeacha kutumia muda wako na marafiki zako ili kusudi uwe na muda mwingi zaidi wa kutumia naye, umemnunulia gauni la gharama na vingine vingi ili apendeze bila kuchoka huwa unabadilisha ratiba zako ili ziweze kuendana na za kwake ili muwe pamoja na kumuonyesha jinsi gani alivyo na nafasi kubwa ndani ya moyo wako, na unafanya yote haya bila ya kumtaka kitu chochote kutoka kwake.
Na hata hivyo ni mara moja tu siku ule ulipokua unaumwa ambapo ulimuomba akupikie ugali na akakuchukulie mishikaki unayoipenda pale uswazi teki awei, ambapo alikataa kwa upole na kukwambia hajui kupika vizuri ugari na wewe ulikubali kwa roho safi maana hupendi kuwa kero kwake.
Sasa turudi kwenye uhalisia.
Rafiki sijui nikuambieje ili unielewe, kaka hapa unatiketi moja tu inayokwenda bila kurudi ambayo kupeleka kwenye nchi ya mvunjiko wa moyo ambapo wapo wapenzi wake wa zamani aliowaacha.
Ni muda wa kumuuliza, "Hivi ni kipi umenifanyia mimi hivi karibuni?".