Mwanamuziki zao la nyumba ya kukuza
vipaji Tanzania ‘ THT’ , Amini Mwinyimkuu
amefunguka kuwa , aliamua kufunga ndoa ya
fasta ili kuuwahi mwezi mtukufu wa
Ramadhani .
Mwanamuziki zao la nyumba ya kukuza
vipaji Tanzania ‘THT ’ , Amini Mwinyimkuu .
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni , Amini
ambaye amemuoa binti aitwaye Farida
Bashiri alisema ilikuwa vigumu kufanya
sherehe kubwa kwani lengo lilikuwa ni
kumuingiza ndani haraka mke huyo ili
amuandalie futari pia .
“Ni kweli nilioa juzi pale Magomeni
Mwembechai , ilikuwa ni ndoa tu na niliamua
kufanya hivyo ili kuuwahi mwezi Mtukufu wa
Ramadhani , ” alisema Amini ambaye ndoa
ilimbadili jina kwa kufungishwa kwa jina la
Namini kufuata mambo ya kinyota .