Latest Updates

Msiba mkubwa wawapata Yaya na Kolo Toure wakiwa nchini Brazil


Masaa kadhaa baada ya timu ya Ivory Coast kupokea kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa Colombia katika mchezo wa kundi C kwenye michuano ya kombe la dunia, mastaa wa timu Yaya na Kolo Toure wamepata habari mbaya zaidi.

Wachezaji hao wanaokipiga katika klabu ya Manchester City ya England, walipokea taarifa ya kifo cha mdogo wao wa kiume ambaye pia ni mwanasoka.

Msiba huo mkubwa kwa Yaya Toure pamoja na kaka yake Kolo Toure umetokea jana jijini Manchester ambapo mdogo wao Oyala Ibrahim Toure alifariki akiwa hosptali The Christie akipewa matibabu baada ya kuugua saratani.


Ibrahim Toure

Ibrahim Toure amefariki akiwa na umri wa miaka 28 na amewahi kuvitumikia vilabu vya

2002-2003: ASEC Mimosas

2003-2006: Metalurh Donetsk

2006-2007: OGC Nice

2009-2010: Al-Ittihad Aleppo

2010-2013: Misr Lel Makasa

2012: Telephonat Beni Sweif (loan)

2013-2014: Al-Safa’ SC