Latest Updates

PICHA FEKI ZA RECHO NA MWANAYE WAKIWA KWENYE JENEZA ZAMUONGEZEA MACHUNGU MUMEWE


MCHUMBA ambaye alifikia hadhi ya mume wa mwigizaji marehemu Sheila Haule ‘Recho’, George Sagunda amefunguka kuwa amechukizwa na watu wasiojulikana kuweka picha feki ya marehemu mitandaoni.

Akizungumza na mtandao huu, Saguda alisema muda mchache baada ya mazishi yaliyofanyika wiki hii, watu wasiojulikana waliweka picha ya marehemu akiwa na mwanaye kwenye jeneza kitu ambacho siyo sahihi.

“Imeniuma sana, wamefojifoji picha na kuweka kichanga ambacho siyo chenyewe kisha kuposti katika mitandao wakidai ni marehemu Recho na kichanga chake, wasifanye hivyo jamani…,” alisema Saguda.