Latest Updates

Serikali yapiga Marufuku tabia ya Trafiki kuvizia magari barabarani kwa kujificha Vichakani



Serikali imepiga marufuku tabia ya askari Polisi wa Kikosi cha Usalama
Barabarani, kuvizia magari katika barabara kuu wakiwana kifaa cha
kupima mwendo kasi wa magari.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Peraira Silima, alisema tabia hiyo ya trafiki ni kinyume cha sheria na
zinaweza kusababisha ajali.Hata hivyo, Silima aliwataka madereva kutii

Sheria za Barabarani ikiwemo kupunguza mwendokasi na kufafanua kuwa,
wakati mwingine askari hutafuta kivuli na hatua hiyo isichukuliwe kuwa
wanavizia magari.Katika swali lake, Ngoye alitaka Serikali ieleze ni
hatua gani zimekuwa zikichukuliwa kuhakikisha madereva wanafuata
sheria zilizowekwa kama inavyofanyika katika nchi nyingine.Ngoye pia
alitaka Serikali ieleze kwa nini madereva wameendelea kutumia magogo,
mawe na majani yenye miba barabarani kuashiria kuwa kuna gari
limeharibika, na wakiondoka wanayaacha na wengine wameendelea
kuendesha magari huku wakisikiliza
simu.Naye Mbunge wa Musoma Mjini,
Vincent Nyerere (Chadema), alihoji kama ni sahihi kwa trafiki kuvizia
magari na kifaa cha kupima mwendo kasi.Akifafanua majibu ya maswali
hayo, Silima alisema trafiki kujifichana chombo hicho na kujitokeza
kusimamisha gari ni kinyume cha sheria kwa kuwa tabia hiyo inaweza
kusababisha ajali.Kuhusu matumizi ya magogo, majani na mawe, alisema
ni kinyume na Sheria na kutaka madereva watumie alama za pembe tatu
ambazo ni nzito na kuachana na alama hizo ambazo ni nyepesi ambazo
hupeperushwa na upepo.Silima pia alionya kuwa Serikali ikombioni
kuanza kuwanyang'anya leseni za udereva
madereva wote ambao
watathibitika kukithiri kwa makosa ya usalama barabarani, na kuzuiwa
kabisa kufanya kazi hiyo.Hatua hiyo itaanza kuchukuliwa mara baada ya
kukamilika na kuanza kwa Mfumo mpya wa Nukta, ambao utaweka kumbukumbu
za makosa ya madereva ambayo itatumika kuwachukulia hatua hiyo.