Latest Updates

VITU 7 AMBAVYO WANAUME WANAFANYA TOFAUTI NA WANAWAKE


1. Kama bahati , Isyu na Martha wakikutana wataitana majina yao kama kawaida, ila upande wa wanaume utasikia we pimbi, mbwa , kimeo n.k

2. Wakitoka out labda for lunch, kwa wanaume hata ikija bill 13,000 utakuta kila mmoja anatupa mezani mwekundu wa msimbazi hata kama wako wanne , Lakini dada zetu wanazama kwenye pochi kwanza wanaibuka na calculator, mwingine simu lazima ijulikane kila mmoja anatoa ngapi.

3. Mwanaume akitaka kununua kitu mara nyingi huishia kulipishwa zaidi ila mwanamke hata nyanya lazima abishane anunue nusu bei

4. Upande wa dressing table , ya mwanaume vitu unahesabu vikizidi sana 6 ila mwanamke unaweza usielewe hata kama vingine huwa anatumia muda gani

5. Mkigombana mwanaume huwa ananuna au kukatisha ugomvi kwa kuchimba bit kali, lakini kwa mwanamke kila neno utakaloongea lazima linazua hoja mpya au mabishano mapya

6. Wanaume hawana tofauti muonekano anavyolala na kuamka ila wanawake ukiwahi kumuangalia before make up utasema sio mwenyewe

7. Mwanamke hujua kila kitu kuhusu watoto wake ila mwanaume hujua wanawake wapya waliohamia mtaani kuliko familia yake.