
Vanessa Mdee akiwa anatikisa media mbali mbali east africa kwa kuanza na video yake mpya ya “Come Over” iliyokuwa gumzo mtaani, Na hivi sasa kama ilikuwa haitoshi kuachia tena Single yake mpya inayoitwa “Hawajui”,
Moja ya single inayongozwa kuimbwa na kila mdau wa muziki hivi sasa. Kali zaidi ya single yake hii ni kile kinachoendelea hivi sasa kwa Wema Sepetu, mbali na kuwa rafiki mkubwa wa Vanessa Mdee, hii nyimbo yake mpya imetokea kumkaa sana akilini,
ni moja ya nyimbo anazozihusudu sana, mapema hii leo Wema sepetu ilibidi afunguke na kuonyesha mapenzi tele yaliyopitiliza kwa mwanadada Vanessa Mdee, ni kuanzia Instagram hadi twitter, ni Wema Sepetu na “Hawajui”, the new hit single in town.