Latest Updates

DR DRE AWAZAWADIA TIMU YA UJERUMANI HEAD PHONES 24 ZA DHAHABU KWA KUTWAA UBINGWA WA DUNIA



Rapper, producer na mwanzilishi wa Beats Electronics, Dr. Dre ni miongoni mwa mashabiki wa timu ya taifa ya Ujerumani iliyotwaa kombe la FIFA la dunia jana (July 13) nchini Brazil.Kutokana na ushindi huo wa Ujerumani Dre ameamua kuipongeza timu hiyo kwa zawadi special ya headphones za dhahabu (special edition 24 carat gold dipped Beats Pro headphones). Wachezaji wote 23 watapata headphones kila mmoja pamoja na meneja wao wa 24.
Naomi Campbell ndiye model aliyehusika katika upigaji picha wa kampeni hiyo ya ‘Golden Project’ ya Beats by Dre. Campbell anaonekana katika picha akiwa amevalia nguo ya rangi ya dhahabu, akiwa ameshika mpira wa dhahabu huku amevaa headphone ya dhahabu.