Latest Updates

#ExclusiveNews || @diamondplatnumz atajwa kuwania tuzo za IRAWMA, Marekani kupitia ‘Mdogo mdogo’, anachuana na Davido




Kwa mara nyingine Diamond Platnumz ametajwa kuwania tuzo nyingine za kimataifa nchini Marekani, ambapo safari hii wimbo wake wa ‘Mdogo mdogo’ wenye miezi miwili tangu utoke umemuwezesha kuingia kwenye tuzo za IRAWMA (International Reggae and World Music Awards).
Wimbo wa ‘Mdogo mdogo’ wa Diamond umeingia kwenye tuzo hizo katika kipengele cha ‘Best African Song/Entertainer’. Kwa mara nyingine Diamond anapambana na Davido anayewania kipengele hicho kupitia wimbo wake ‘Aye’.





Nominees wengine wa Afrika katika kipengele hicho ni “Bundeke” – AwiloLongomba (Congo), “Mama Africa” – Bracket (Nigeria), “Tam Tam” – Willy Paul Msafi (Kenya), “Sitya Loss” – Eddy Kenzo (Uganda).


DABO

Diamond hataipeperusha bendera ya Tanzania peke yake, msanii wa dancehall DABO pia anawania kipengele cha ‘Best New Entertainer’.

Tuzo zitatolewa Jumamosi October 4, 2014 Coral Springs center For The Arts, Florida, Marekani.

Upigaji wa kura tayari umeanza kupitia www.irawma.com, ili kumpigia kura Diamond fuata link hii (http://irawma.com/irawma_vote2014), kisha tafuta kipengele cha ‘Best African Song/Entertainer’, na kumpigia kura DABO tafuta kipengele cha ‘Best New Entertainer’.

Kuhusu IRAWMA: