![](http://2.bp.blogspot.com/-MFDpP3rmKtQ/U_zz0v1qKqI/AAAAAAAAjVg/-4e-c4Zs8xI/s640/Jamaa%2Bwa%2BNyoka_full.jpg)
Ruben Ramirez mwenye miaka 41 ameamua kujitolea kuingia porini huko Florida, Marekani kupambana na nyoka wakubwa ambao walivamia eneo hilo tangu mwaka 2000 na kula wanyama mbalimbali katika maeneo hayo.
Ramirez ambaye ni mwenyeji wa eneo hilo ameeleza kuwa wakati anakuwa, yeye na baba yake walikuwa wakienda porini kuangalia wanyama mbalimbali lakini tangu chatu hao walipovamia eneo hilo hawaoni tena wanyama hao na ndio sababu akaamua kuwapunguza.
Mwanaume huyo hupigana mieleka na chatu hao na kuwashika wakiwa hai kisha kuwakabidhi kwa maafisa wa wanyama pori wanaowatoa katika eneo hilo kwa lengo la kusaidia wanyama kukua.
![](http://2.bp.blogspot.com/-O76I5UAXZS8/U_zzzPW0JjI/AAAAAAAAjVY/dIgD6ivmTE0/s640/JAMAA.jpg)
Pamoja na hatari kubwa anayokabiliana nayo, anadai kuwa hufurahia sana kupigana mieleka na nyoka hao.