4
Mwili wa Rashid Athuman ukiwa unaning’inia katika kitanzi ambacho alikifunga chooni kabla ya kujinyonga kasha kujifungia chooni.
Mwili wa Rashid Athuman ukishushwa na wasamaria wema kutoka kwenye kitanzi kwa kwa kushirikiana na Jeshi la polisi.
Mwili wa Rashid Athuman ukiwa unahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhiwa maiti katika hospital ya Peramiho.
Hiki ni chumba ambacho marehemu alikuwa amepanga na kinachoonekana ni kitanda ambacho alikuwa anatumia kulala yeye na mke wake .
Mke wa marehemu Lucy Adam (24) akiwa amembeba mtoto wake Yoweri Rashid (02) mgongoni.Na Oswad Ngonyani Peramiho - Songea
Ikiwa imepita siku moja tangu mazishi ya Fundi maabara mstaafu wa Hospitali ya Peramiho Bwana Frederick Mgaya (60) ambaye alifariki kwa kujinyonga alhamisi iliyopita hapa Peramiho, mtu mwingine tena aliyetambulika kwa jina la Rashid Athuman (32) amekutwa amejinyonga katika choo cha nyumba aliyokuwa akiishi.
Bwana Rashid Athuman ambaye ni mkazi wa Usangu Jijini Mbeya amejinyonga kwa kutumia shuka majira ya saa Saba za usiku baada ya kumuaga mke wake Bi Lucy Adam (24) kuwa anakwenda chooni kujisaidia ambapo alikwenda kukamilisha mpango wake huo.
Taarifa kutoka kwa mke wake huyo zinaeleza kuwa enzi za uhai wake Bwana Rashid Athuman alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu, tatizo lililowafanya wachukue uamuzi wa kuja Peramiho kwa ajili ya matibabu.
Bi Lucy anazidi kutanabaisha kuwa walifika Peramiho tarehe 19 Mwezi Julai 2014 na kupata chumba cha kupanga katika Kitongoji cha Namihoro jirani na Stendi Kuu ya Peramiho katika nyumba ya Cosmas Chidumule ambapo tangu wakati huo waliendelea na maisha yao wakiwa wakisaidiwa chakula na majirani waliokuwa na mapenzi mema.
“Tangu jana asubuhi nilishinda vizuri tu na marehemu mume wangu ambapo mishale ya saa tatu za usiku tulienda kulala. Muda mchache baadaye nilipitiwa na usingizi mpaka majira ya saa saba za usiku ambapo marehemu aliniamsha na kunieleza kuwa alikuwa anakwenda uani kujisaidia ambapo baada ya yeye kuelekea uani mimi niliendelea kulala” Alisema mke huyo wa marehemu.
“Baada ya muda mrefu kupita pasipo marehemu kurudi nikaamua kuamka na kutaka kuufungua mlango wa chumbani lengo hasa likiwa kwenda uani kujua sababu ya mume wangu kuchelewa kurudi. Nilishangaa kuona mlango umefungwa kwa nje na ikanibidi nitumie kisu ili kuweza kuufungua mlango huo ambapo nilifanikiwa na kwenda uani ambapo nilikuta mlango wa uani ukiwa umefungwa kwa ndani kitu kilichonifanya niusukume kwa nguvu na kumkuta mume wangu akiwa ananing’inia huku akiwa amekwishafariki” Alimalizia mjane huyo.
Mjane huyo ameishi na marehemu kwa muda wa miaka mitatu na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume, Yoweri Rashidi (2) ambapo uchunguzi zaidi kuhusu chanzo cha kifo hicho bado unaendelea.