Latest Updates

AIBU JAMANI..MAMBO YA NDANI YA SHUKA MOKO...MNAFIKI KAA PEMBENI..wakubwa tuuuuu



Hehehe… heeeeee, heiiiya, acha nicheke miye mwana wa marehemu, sijui
wazazi wangu huko waliko wako katika hali gani, nawaombeakwa Mwenyezi
Mungu awape kivuli chake sikuya kiama.Waweza kuona nacheka ukadhani
labda nimejawa na furaha, kumbe nafsi yangu imejaa karaha, imekereheka
kama siyo kukereheshwa.Kuna watu wengine kwa kweli kila kitu watende
wao wakitenda wenzao huwa mwao, hutaka kuicheza ngoma hata kama siyo
ya kwao, upo?Hivi inaingia akilini mama mtu mzima kutaka kuingilia
ndoa ya mwanaye? Tuchukulie mfano ni wewe mama ungekuwa na mtoto wa
kike, ndoa yake ikawa inaingiliwa na mzazi mwenzako
ungefurahi?Nalisema hili kwenu nyie wenye tabia hii kwa kuwa huu ndiyo
mwarobaini wenye ladha chungu, lakini ndani yake unapata dawa ya
kutibu maradhi yako ya nyongo.Kwa nini leo nimeamua kuyasema haya?
Jamani kuna shoga yangu mmoja kanijia mikono kichwani machozi
churuchuru nikadhani labda amefiwa, alichonieleza nilibaki mdomo wazi
kama siyo kupigwa na bumbuwazi.Eti, mwanaye amekuwa akiendeshwa na
mkewe kama gari bovu. Yaani mkwewe amekuwa ndiye kinara wa nyumba na
mtoto wake hafurukuti wala hatikisiki.Kila siku mama anamwambia
mwanayeubaya wa mkewe lakini mtoto wala hajali, maneno yanaingia sikio
hili yanatokea lile, hasikii kitu juu ya mkewe.Siku moja, shoga yangu
akapewa na mwanayemaneno makavu, kuwa hawezi kuachana na mkewe kama
anavyotaka yeye, hilo likamuumampaka akaamua kuja kuniangushia
kilio.Mmh, makubwa limao alambe mwingine weweukunje uso kama ngozi ya
goti, leo nataka niwaeleze nyie kina mama mnaokosa kazi na kufuatilia
ndoa za watoto wenu, jamani acheniii.Hamuoni aibu, mama mkwe kuacha
kazi na kuwa kiguu na njia kufuatilia ndoa za watoto wenu kama mkia wa
ng'ombe. Kwanza kwa mila na desturi za Kitanzania ni matusi kufanya
hivyo.Mama mtu mzima huna kazi, unafuatilia nyendo za mkweo, jioni
mwanao akirudi unampa 'full data', cha ajabu mwanao haoneshi
chochote kutokana na madai yako, unakasirika.Mwanao wa kumzaa
mwenyewe akikupuuza unamuona hafai na hana maana, unaanza kuzunguka
mitaani na kusema kuwa, mwanao hajaoa bali kaolewa.Ni jambo la
kushangaza kwa mtu mwenye akilizake na aliyedumu katika ndoa kufanya
ujinga huo.Tunajua kwamba kuna wazazi walioshindwa kuziongoza ndoa zao
kwa kukosa uaminifu, lakini leo ndiyo hao hao wanaokosa uso wa haya na
kuanza kufuatilia maisha ya wakwe zao kisha kupelekaumbeya kwa watoto
wao.Eti, watoto wao wakikataa ushauri wao wanataka kuwatolea radhi,
mmh! Jamani nyie nani aliwatolea radhi? Mbona yenu mengi tunayajua
lakini hatusemi?Siye tumenyamaza kwa kuelewa kwamba ndoani siri ya
watu wawili, tunafahamu pia kuwa kila lenye mwanzo lina mwisho wake,
kwa nini tutake kuitwa wachawi kwa jambo ambalo ukweli unaweza
kubainishwa na mhusika mwenyewe?Heee! Kama mke na mume kuna anayefanya
uchafu ni mmoja kati yao ndiye anayeweza kuubainisha kwa kuwa wote
wana macho watayaona na kutoa hukumu bila kumlaumu mtu yeyote ya nini
siye tuyaingilie?Tafadhali, shoga usiwe kimbelembele kama mfuko wa
shati kutaka kuvunja ndoa ya mwanao, unajua mwanao anafanyiwa nini na
mkweo? Unajua analishwa nini? unajua anapumbazwa kwa pumbazo gani?
Alaaaa! Acha ushakunaku.Wewe kama ungefuatiliwa hivyo ndoa yako
ingedumu? Yako ni yako na ya wenzako pia yako.Napenda kukwambia wewe
unayebinua midomo kama samaki chuchunge na wenzako kuwa msipende
kuingilia mambo ya watu wanaojifunika shuka moja, mtakuja kupatwa na
aibu