Latest Updates

HII NDO SABABU KUU YA ANTI LULU KUDENDEKA NA SHOGA...SOMA MWENYEWE


MTANGAZAJI chakaramu Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amenaswa akiwa hoi kwa kilevi na kuwaacha wadau wakisema ‘kazi ni kwako’.
Kituko ni kwamba, Aunty Lulu alifakamia pombe hizo zilizompeleka hali ya ‘u-tilalila’ katika kipindi hiki ambacho anakabiliwa na mitihani ya kumaliza masomo ya uandishi wa habari ngazi ya stashahada.



Staa huyo aliyeanza ‘kuhiti’ tangu akiwa na umri mdogo, alinaswa na kamera zetu usiku wa Jumatano iliyopita ndani ya Club Bilicanas, Dar es Salaam.


Ilikuwa saa 6:39, paparazi wa Risasi Jumamosi alimtia machoni Aunty Lulu kwa mara ya kwanza ndani ya klabu hiyo, kulikokuwa na shoo ya Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’.

Wakati huo, staa huyo alikuwa akirandaranda mfano wa mtu aliyekuwa akitafuta sehemu ya kujiegesha.

Baada ya kuzunguka kwa dakika mbili hivi, Aunty Lulu alitenga makalio jirani na moja ya kaunta za klabu hiyo na kuanza kukata monde a.k.a maji ya mende ambayo yalimchakaza na kumuacha hoi.

Kabla hajazimika, Aunty Lulu alifanya vitu viwili kwa zamu akiwa tayari rojorojo, kunywa pombe kwa fujo na kuchangamka kwa muziki wa Twanga, hivyo kukata mauno ‘kama hana akili nzuri’.


Kama ilivyo kwa msemo, ‘ulevi noma, funda moja tu la ziadalinaweza kukuumbua’ ndivyo mambo yalivyomtokea puani Aunty Lulu, kwani mwisho alikuwa taabani na kufanya yasiyo na heshima.



Moja ya matukio ya kilevi aliyoyafanya ni kumvamia jamaa mmoja (anayedaiwa siyo riziki, pichani mbele) na kudendeka naye bila woga kabla ya kulala fofofo kwa kuugeuza ubao wa kaunta ndiyo kitanda cha chumbani kwake