MWIGIZAJI nyota wa filamu, Rose Ndauka ameibuka na kukanusha vikali uvumi uliozagaa kuwa uchumba wake na Malick Bandawe umevunjika na kusema siyo kweli kwani bado upo ngangari kuliko kawaida.
Mwigizaji nyota wa filamu Bongo, Rose Ndauka akipopzi. Akistorisha na gazeti hili juzikati, mwigizaji huyo anayeishi na mchumba wake huyo, alisema uvumi huo hauna msingi kwa sababu asubuhi ya siku hiyo (Jumatatu) alikuwa amemnyooshea nguo alizovaa wakati akielekea kazini kwake.
Rose Ndauka akiwa na mpenzi wake Malick Bandawe. Awali, kulikuwa na madai ya kuwepo kwa mtafaruku baina ya wawili hao na kudaiwa kuachana kutokana na mmojawapo kulala nje siku tatu, kitendo kilichochochewa na kuonekana kwa Rose akiwa peke yake wakati wa fainali za kumtafuta msanii chipukizi zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City wiki iliyopita.