Ushuhuda wa huyu dada inawezekana ukakufumbua macho na kujua wapi sehemu sahihi ya kuelekea na kujua nini unachotakiwa kukifanya kama umeshaanza kujiandaa safari ya kwenda Dubai.
Wimbi kubwa la ukosefu wa ajira nchini bado ni tatizo kubwa ambalo hupelekea wengine wanaposikia kuna kazi sehemu huamua kwenda moja kwa moja kufatilia kuhusu ajira hiyo.
Gea Habib ameongea na msichana huyu amabye kiasili yeye ni Mwenyeji wa Moshi na amesimulia stori yake nzima na vitu walivyokuwa wanafanyiwa wakati yupo huko Dubai.