Latest Updates

Meek Mill atangaza ujio wa collabo yake na Davido, Wizkid afurahia habari hiyo hadharani


Rapper Meek Mill wa Marekani ambaye pia inaaminika kuwa ni mpenzi wa Nicki Minaj, ametangaza ujio wa collabo yake na staa wa Nigeria Davido kupitia Twitter, japo haijawekwa wazi yupi kati yao aliyemshirikisha mwenzie.



Rapper huyo alitweet “Davido x meek mill coming soon too! #aye”



Davido hakukaa kimya, alithibitisha ujio wa collabo hiyo kwa kuretweet na kujibu mbele ya tweet ya Mill kwa kuandika, “BADDEST!!



Habari hizo njema ziliwafurahisha si tu mashabiki wa Nigeria bali hata aliyekuwa adui wa zamani wa Davido, Wizkid.

Kwa kuonesha kuwa sasa urafiki wa Wizkid na Davido si wa mashaka tena, Wizzy afurahia habari hiyo kwa kupost tweet za Meek Mill na kuandika: “Naija to the world! @daddymiliano x @davidoofficial !”



Davido naye alimjibu Wizkid:



Hiki ndicho Watanzania wengi wanatamani kuja kukiona kikitokea kwa Diamond na Alikiba, kwa faida ya muziki wa Tanzania.