Latest Updates

HATOKI MTU HAPA: HATIMAYE SIMBA WAMPIGA PIN HAMIS TAMBWE KWENDA CLUB NYINGINE..!




Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe.HATIMAYE mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe, ambaye hivi karibuni alihusishwa kutaka kuikimbia klabu hiyo na kwenda kujiunga na timu nyingine za ligi kuu, amepigwa pini na klabu hiyo baada ya kuhakikishiwa neema msimu ujao.

Tambwe ambaye ni raia ya Burundi na ambaye ndiye amekuwa msaada mkubwa wa timu hiyo msimu huu baada ya kuifungia mabao 19 kweney ligi, amekuwa akihusishwa na taarifa za kujiunga na Yanga na Azam FC lakini ameelezwa kuwa kuna kundi moja, Championi inafahamu kuwa ni Friends of Simba, linaweza kuingia madarakani na kumtimizia mahitaji yake yote.


Mwenyekiti wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage. Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe alisema kuwa hivi karibuni uongozi wa klabu hiyo umemtaka atulie na asiwe na haraka za kutaka kuondoka katika kikosi hicho, kwani mambo mazuri yanakuja.

Alisema katika mazungumzo aliyofanya hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alimhakikishia kuwa mambo yake yatakwenda sawa bila tatizo lolote hivyo anatakiwa kuvumilia mpaka uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakapomalizika na viongozi wapya wakipatikana.

“Aliniambia hata kama nikiwa nyumbani Burundi atakuwa akinijulisha kila kitu kitakavyokuwa kinaendelea huku, hivyo nisiwe na wasiwasi mambo yangu yatashughulikiwa, kwani anaamini uongozi utakaoingia madarakani, utakuja na mikakati mizuri zaidi kwa kuwa anaamini wengi wao ni watu wenye fedha.
“Kutokana na hali hiyo kwa sasa siwezi sema kama nitaondoka Simba au nitabakia lakini kila kitu kitajulikana hapo baadaye, acha niwasikilizie kwanza viongozi hao, nimeelezwa na mtu mwingine kuwa kuna kundi moja linatwa Friends lina watu wenye uwezo sana linaitaka timu nafikiri ni watu ambao tutawezana,” alisema Tambwe ambaye mkataba wake wa kuitumikia klabu hiyo unamalizika mwakani.

-CHAMPION