Latest Updates

MAVAZI YA NUSU UTUPU MASTAA WA BONGO..BATULI AFUNGUKA KIKUBWA ZAIDI...!!



MWIGIZAJI mwenye mvuto Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amewataka wasanii wenzake wabadilike na kuvaa kama yeye kwani muda wa kuvaa nusu utupu umepitwa na wakati.


Mwigizaji mwenye mvuto Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’Akizungumza na paparazi wetu baada ya kutupia picha yake aliyovaa gauni refu mtandaoni, Batuli alisema: “Muda wa kuvaa utupu umepita, wasanii tunapaswa tubadilike kwani kila siku tumekuwa tukisemwa vibaya na jamii.”


Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ akiwa kwenye pozi.Batuli aliongeza kuwa, kama kila msanii wa kike atavaa kiheshima, wataheshimiwa na kuwa mfano wa kuigwa.