Latest Updates

AIBU KUBWA DAR: MSANII AFUMWA LIVE AKINGONOKA NA DENTI UFUKWENI...!



Aibu nzito! Msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Venas John Bebu ‘Bebuz’ amenaswa laivu akivunja amri ya sita (kuzini) na mwanafunzi wa sekondari ufukweni.


Msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Venas John Bebu ‘Bebuz’ afumwa akivunja amri ya sita ufukweni Tukio hilo la aibu lilijiri wiki iliyopita mishale ya saa 8:00 usiku kwenye Ufukwe wa Coco, Dar ambapo polisi jamii walimnasa jamaa huyo aliyedaiwa ni swahiba mkubwa wa mwanamuziki, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ ambao hivi karibuni walitoa kibao kipya kijulikanacho kwa jina la Bunyerobunyero.
Mara baada ya kunaswa, Bebuz alianzisha varangati kubwa lakini polisi jamii walimtuliza kwa virungu kisha kumfunga pingu na kumtaka atulize mzuka atoe ushirikiano vinginevyo angeumia.
Kijana huyo alitulia kwa muda lakini alipowaona OFM wakipiga picha, alilianzisha tena na kutaka kuvunja kamera huku akitamba kuwa alikuwa na uwezo huo.
Hata hivyo, OFM walikuwa makini kama kawaida yao.


Wakiwa chini ya ulinzi wa kachelo wa polisi Ufukwe wa Coco umekuwa ukilalamikiwa kwamba hukutanisha watu wenye malengo mbalimbali lakini wanaokwenda kwa ajili ya kufanya ufuska usiku ni wengi hasa siku za wikiendi ambako kunakuwa na burudani ya disko.
Kikosi maalum cha kufichua maovu OFM (Opereshen Fichua Maovu) cha Global Publishers kilipiga kambi katika ufukwe huo kwa muda wa wiki moja na kushuhudia maovu yanavyofanyika.

Pia OFM ilibaini kuwa katika ufukwe huo kumekuwa kukifanyika vitendo ambavyo siyo vya kiustaharabu ambapo watu wamekuwa wakifanya ngono katika vichaka na kwenye maji.
Katika siku za hivi karibu, machangudoa wamekuwa wengi ufukweni hapo na baadhi yao ni vibaka ambao wamekuwa wakitoka nduki na nguo za wanaume huku wakisachi na kuchukua kila kitu.

-GPL