Good news kuhusu ushindi wa timu ya soka ya Tanzania U-15
Tanzania inaendelea kufanya vizuri kwenye michezo ya Afrika kwa vijana (AYG) kwenye mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 baada ya leo (Mei 23 mwaka huu) kuwachapa wenyeji Botswana magoli mawili bila.
Magoli kwenye hii mechi iliyochezwa uwanja wa SSKB jijini Gaborone yalifungwa na David Uromi dakika ya sita huku Anthony Amede akitupia la pili kwenye dakika ya 46.
Katika mechi yake ya kwanza, Tanzania ilitoka sare ya bao 1-1 na Mali na sasa vijana hawa wa JK watacheza mechi ya tatu kesho kutwa (Mei 25 2014) vs Swaziland na watakuwa tena uwanjani Mei 27 2014 vs Nigeria wakati mechi ya mwisho itafanyika Mei 29 2014 mwaka huu dhidi ya Afrika Kusini
St
Posted