UNYAMA wa kutisha! Gasto Edward (32) amemkata mkewe Mwelu Raymond sehemu zake za siri, Risasi Jumamosi lina simulizi hii ya kusikitisha. Tukio hilo lilitanguliwa na kumpiga mkewe huyo na kipande cha nondo kichwani hali iliyosababisha apoteze fahamu papo hapo na kutekeleza azma yake.
Bwana Gasto Edward na mkewe ambaye anadaiwa kumkata nyeti zake.Imeelezwa kuwa, tukio hilo lenye sura ya majonzi, lililovuta hisia za watu wengi lilitokea Jumatano ya wiki hii, huko King’azi, Kwembe – Mbezi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
KISA CHA YOTE
Habari zilizopatikana eneo la tukio zinadai kuwa, chanzo cha unyama huo ni wivu wa kimapenzi ulioingilia ndoa hiyo, ambapo Gasto alimtuhumu mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine anayeishi Temeke aliyejulikana kwa jina la Mgogo.
Chanzo chetu cha kuaminika, kwa sharti la kutotajwa gazetini kilisema: “Mwelu na Gasto wametoka mbali, wameishi kwa muda mrefu na wamebarikiwa watoto wawili, sema siku za hivi karibuni, Gasto alianza kumtuhumu mkewe kuwa anatoka nje ya ndoa.
Wananchi wakizulu eneo la tukio. “Tena siyo tuhuma, anasema alikuwa akimwambia wazi kuwa ana mwanaume wake Mgogo ambaye yupo Temeke. Jamaa alikuwa analalamika kuwa mkewe alifikia hatua ya kumwambia amuache ili aende kwa mwanaume huyo anayejua kutunza.”
Akaongeza: “Unajua katika hali ya kawaida, kama ni kweli mke alikuwa akimwambia mumewe maneno ya hovyo kama hayo, yanaumiza. Ndiyo maana jamaa akaona kwa sababu chanzo cha yote ni penzi, akamkata nyeti zake.”
MJUMBE ANAFAFANUA
Mjumbe wa Mtaa wa King’azi, Amani Abdallah alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa Gasto, mwezi mmoja uliopita na kufanikiwa kusuluhisha.
“Ni kweli walikuwa na tofauti na hili suala lilinifikia hata mimi. Gasto alikuja kulalamika kuwa mkewe siyo mtulivu na anamwonyesha dharau. Lakini tulisuluhisha yakaisha. Jana (Jumatano) ambapo tukio lilitokea, yule mkewe alikuja kulalamika kuwa mumewe amebadilika.
“Alisema amemuona akinoa kisu asubuhi, usiku ugomvi ukatokea akaamua kuja kulala kwangu, lakini baadaye akaniaga anakwenda kulala kwa jirani yao mama Mbonde, huko ndipo mumewe alipokwenda kumchukua na kumfanyia unyama huo.”
WOSIA MZITO
Baada ya tukio hilo, Gasto alitoroka lakini aliandika wosia uliomtaja mrithi wa mali zake kuwa ni watoto wake Edward na Editha ambapo alimchagua kabisa msimamizi wao kuwa ni mdogo wake aitwaye Kiriani.
Katika barua hiyo, Gasto alisema anakwenda kujiua kwa sababu amechoshwa na dharau za mkewe, ndiyo maana akaamua kuondoa sehemu zinazompa kiburi.
Kesi ya Gasto imeripotiwa katika Kituo cha Polisi Kwa Yusuph na kufunguliwa jalada nambari KWR/RB/4716/14 – KUJERUHI.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura alipopigiwa na Risasi Jumamosi ili kuelezea tukio hilo, alikiri kupokea taarifa, akasema bado wanafuatilia.
-RISASI
Kesi ya Gasto imeripotiwa katika Kituo cha Polisi Kwa Yusuph na kufunguliwa jalada nambari KWR/RB/4716/14 – KUJERUHI.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura alipopigiwa na Risasi Jumamosi ili kuelezea tukio hilo, alikiri kupokea taarifa, akasema bado wanafuatilia.
-RISASI