Johari:Ray Hawezi Kumuoa Chuchu Hans Hata kwa Dawa
Blandina Chagula ‘Johari’, juzikati alifunguka kwamba watu waachane na kusikiliza habari za matapeli wa mapenzi, maana suala la Vicent Kigosi ‘Ray’, kumvisha pete mchumba wake wa sasa Chuchu Hans si la kweli na kwamba huo ni utapeli
Akizungumza Ijumaa Mei 13, mwaka huu Johari alisema hana taarifa zozote za Ray kumvisha pete Chuchu na wala hatarajii kusikia tukio la wawili hao kuoana limefanyika.
“Mmh…unasema Ray kamvisha pete Chuchu...! Hakuna jambo kama hilo wewe, achana na matapeli maana hakuna ishu kama hiyo na Ray hawezi kuoa kwa muda huu.”
“Kwani suala la kumvisha pete na kutoa mahari lilifanyikia wapi maana kama kweli kuna mazingira hayo basi atakuwa kafanya kwa kificho sana.”
Posted