MSANII SARAFINA WA MIZENGWE NAYE YUPO HOI HOSPITALINI, KILICHOMSIBU KIPO HAPA
STAA mkongwe wa vichekesho kutoka kundi la Kashikash Bongo Jessica Kindole ‘Safina’ akiwa hoi hospitali
=======
Safina ambaye ana ujauzito wa miezi 7, alifikishwa katika Hospitali ya St. Monica iliyopo eneo la darajani, Manzese juzikati ambapo alilazimika kulazwa baada ya madaktari kuona mwili wake umepoteza nguvu.
Kwa mujibu wa mtu aliyekuwa akimuuguza (hakupenda jina lake lichorwe gazetini), staa huyo alipopimwa na daktari, aligundua kuwa ana ugonjwa wa UTI pamoja na ugonjwa huo wa kuendesha damu huku ndugu zake wakimuombea usiku na mchana.
Baada ya waandishi wetu kuzinyaka taarifa hizo, walimpigia simu staa huyo ambapo alipopatikana alisema anamshukuru Mungu anaendelea vizuri na kudai alikuwa anasumbuliwa na malaria pamoja na kutapika.
Jessica Kindole ‘Safina’akiwa na msanii mwenzie.
“Nashukuru kwa kunijulia hali, sasa naendelea vizuri na mtoto anaendelea vizuri namshukuru Mungu,” alisema Safina.
Nesi mmoja ambaye pia hakupenda jina lake liandikwe gazetini, aliwaambia waandishi wetu kuwa mtoto aliye tumboni alikuwa hachezi kwa muda mrefu lakini mpaka tunakwenda mtamboni, alikuwa akiendelea vizuri.
Imeandikwa na Hamida Hassan na Gladness Mallya, GPL.
Posted