Latest Updates

Muziki wa dance umepata pigo jingine leo, ni hiki kifo cha Mwimbaji Amina Ngaluma ‘Japanese’





Kwenye hii picha Marehemu Amina enzi za uhai wake aliiweka facebook na kuandika ‘bila giza tusingezijua nyota’

Amina Ngaluma ‘Japanese’ ni miongoni mwa waimbaji ambao waliipa umaarufu sana bendi ya African Revolution ‘Tam tam’ kupitia wimbo wa Mgumba na baadae kujiunga na bendi ya Double M Sound ambapo mpaka anafariki alikua nchini Thailand akifanya kazi na band ya Jambo Survivors.

Amina amefariki May 15 2014 saa sita mchana baada ya kuumwa kwa siku nne ambapo mume wake alipozungumza na millardayo.com amesema kiongozi wa band yao huko Thailand alimwambia Amina alilazwa hospitali kutokana na maumivu makali ya kichwa.


Ilipofika Jumapili ndio ilibidi alazwe hospitali baada ya kuzidiwa akapumzishwa na hivyo akawa hawezi tena kupokea simu ambapo mara ya mwisho kuongea na mume wake ilikua ni Ijumaa iliyopita.

Amina alikwenda Thailand miezi nane iliyopita baada ya kuongeza mkataba kuifanyia kazi bendi hiyo ya Watanzania ambayo ina mkataba mrefu wa kupiga nchini humo.




Hii ni moja ya status zake za mwishomwisho facebook

Msiba upo Kitunda Machimbo kipunguni B nyumbani kwao na kesho ndio watajua taratibu za kuuleta mwili wa marehemu nchini Tanzania.