NISHA AELEZA JINSI SANI WALIVYOMTAKA AWALIPE MIL 100
Unakumbuka magazeti ya zamani ya Sani na katuni zake za Zena na Betina? Muigizaji wa filamu, Salma Jabu aka Nisha alikataliwa kuitoa filamu yenye jina la Zena na Betina na uongozi wa gazeti la Sani kwa kile walichodai alitumia majina yenye haki miliki ama lasivyo alipe shilingi milioni 100 kupata haki hiyo.
Hata hivyo, Nisha ameiambia BK kuwa mambo yote yameenda sawa na filamu hiyo itatoka.
“Kweli gazeti la Sani walinitaka nitoe faini ya milioni 100 baada ya kudai nimetumia jina la katuni wao ambao wanatumika kwenye gazeti lao, lakini kwa bahati mzuri tulikaa chini na kulimaliza suala hili, walichokujagundua katuni za kwenye gazeti lao na filamu yangu labda vimefanana majina ,lakini stori ziko tofauti kabisa, kwahiyo wadau wakae mkao wa kula filamu ya Zena na Betina itatoka tarehe 29 mwezi huu,” alisema.
Katika hatua nyine, Nisha alidai mwaka huu atawafanyia watu surprise ya ndoa yake. “Bado sijaolewa ila inshallah soon, surprise nawaletea karibuni,nikisema karibuni na maana ,sema inshallah,” alisema.
Posted