BREAKING NEWS: WATU SITA WAFARIKI KWA AJALI ILIYOHUSISHA BASI NA LORI
Basi la Ndenjela lililogongwa na kupinduka eneo la Nanyala Mbeya
Lori lililosababisha ajali likiwa limepinduka upande mwingine baada ya kuligonga basi la Ndenjela
Adelina Malipesa moja wa majeruhi katika ajali hiyo ambae pia aliporwa pesa na vibaka waliojifanya wasamaria wema
Emmy Charles moja kati ya majeruhi akiwa katika hospitali ya Ifisi
Watu Sita wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni Ndejela Express lenye namba za usajili T 257 CMP aina ya TATA likiendeshwa na Dereva wa kike Vailet Mbinda(31) mkazi wa Sokomatola kugongwa kwa nyuma na roli la mizigo kisha kupinduka Kijiji cha Nanyala Kata ya Nanyala wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa tisa alasiri barabara ya Tunduma/Mbeya ambapo roli lenye namba T 369 AWM aina ya SCANIA likendeshwa na Dereva asiyefahamika likiwa katika mwendo kasi liligonga basi kwa nyuma kisha magari yote mawili kupinduka.
Miongoni mwa waliofariki ni Zainabu Mohammed aliyekuwa kondakta wa basi hilo linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Sumbawanga kila siku, Padri Barnaba Lwemba 35 wa Morogoro Emmanuel Philipo 1 wa Sumbawanga Neusta Jacob Mafuga 27 wa iringa Milika Mbingamno 38
Mwanaume mmoja na Mwanamke mmoja walifariki eneo la tukio na wawili walifariki wakati wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya wakati majeruhi wanane walikimbizwa Rufaa kutokana na hali zao kuwa mbaya.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na juhudi za kumtafuta Dereva wa roli zinaendelea.
Aidha amewataka wamiliki wa magari na madereva kuyafanyia matengenezo na ukaguzi wa mara kwa mara magari yao ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali Teule ya Wilaya ya MbeyaIfisi, Sikitu Mbilinyi amewataja majeruhi kuwa ni Dereva amewataja majeruhi kuwa ni Fred,Maiko Malema(16),Justin Komb(24),Amir Ramadhan(26),Nausi Bakari(28),Jackson Kambo(19),Anoria Ndezi(13) na Lucy Edson(17).
Mbilinyi amewataja wengine kuwa ni Groly Paul(27),Moyo Safi(1),Rahma Peter(3),Mary Kitine(57),Mariam,Karen Naiman,Mecy,Adelina Malipesa(52),Suzana Athas(35),Adelina Essau(28),Frola Essau(64) na Emmy Charles(21).
Wengine waliolazwa ni pamoja na Diana Jumbe(19),Esther Seleman(21),Paul Mayeta(45)ambaye ni Dereva msaidizi,Bahati Julius(33) na Joeph Komba(34).
Kwa mujibu wa Muuguzi Mkuu hali za majeruhi zinaendelea vizuri na wanafanya kilajitihada za kuokoa maisha yao na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kuchangia damu kwani Hospitali hiyo ina uhitaji mkubwa kutokana na kuwa karibu ya barabara kuu na ajali zinazojitokeza mara kwa mara ingawa hupatiwa damu kutoka Benki ya Damu salama.
Hata hivyo baadhi ya abiria wamelalamikia kitendo cha baadhi ya wananchi wa Nanyala badala ya kusaidia majeruhi walikuwa wakiwapora mizigo,simu na fedha pia waliokuwa na vito vya thamani kama heleni.
Jackson Kambo ambaye ni mmoja wa wahudumu wa basi hilo amesema kuwa kama ushirikanowa wananchi hao wangeutoa mapema kondkta wake aingefariki lakini badala ya kusaidia walikuwa wanan’gan’gania mkoba wa fedha hadi walipofanikiwa kuchukua fedha ndipo walianza kutoa msaada marehemu akiwa amelaliwa mkono na basi.
Kambo amesema kama si juhudi binafsi Dereva wa basi angepoteza maisha kutokana na kubanwa na mkanda hivyo kulazimika kuukata na kuanza kusaidia kuokoa abiria wengine
Posted