KIJIJI CHAENDESHA MSAKO KUWANASA WALAWITI
WANANCHI zaidi ya 500 wa Kijiji cha Moivaro na Chekereni katika Kata ya Moshono, wilayani Arumeru wamelazimika kuendesha oparesheni ya kuwasaka wanaume wanaolawiti wanaume wenzao baada ya kugundulika sehemu kubwa ya wanaume katika kijiji hicho wamelawitiwa.
Wananchi wa Kijiji cha Moivaro na Chekereni katika Kata ya Moshono, wilayani Arumeruwakiwa kwenye kikao cha kuwasaka walawiti
Inadaiwa kuwa kikundi hicho cha watu zaidi ya saba kimekuwa kikiwalawiti wanaume wenzao wa rika mbalimbali katika Kijiji cha Chekereni na Moivaro na kuwasababishia maumivu makali sehemu ya makalio.
Hatua hiyo ilifuatia hivi karibuni mwanaume mmoja mwenye miaka 42 (jina tunalo) kulawitiwa hadi kupoteza fahamu na kukutwa mtaroni akiwa hajitambui.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo juzi (pichani), mwenyekiti wa mkutano huo, Johnfas Molleli au Medoli
Molleli alisema kuwa upo uwezekano mkubwa kwa wanaume wengi katika kijiji hicho walishalawitiwa ila wamekuwa waoga kujitokeza kutokana na aibu.
Molleli alisema kama kuna wanaume waliokumbwa na kadhia hiyo kuweka uwoga pembeni na kujitokeza kwenda kupima hospitalini ili kubaini iwapo hawajaambukizwa magonjwa ya zinaa.
“Hapa kwenye mkutano wapo wanaume wengi ambao wamelawitiwa na hilo kundi ila mmekuwa waoga kujitokeza. Ninachotaka kuwaomba kapimeni afya zenu ili mjitambue kama mmeambukizwa magonjwa ya zinaa,’’ alisema mwenyekiti huyo.Katika oparesheni hiyo, wananchi walifanikiwa kuwatia mbaroni vijana
wanne, Richard, Stephano, Furaha na Paulo huku wengine wawili, Thobias na mwingine aliyefahamika kwa jina la Baba wanaendelea kusakwa wakiwa wote ni wakazi wa vijiji hivyo.
Molleli alisema kuwa kabla ya oparesheni hiyo watuhumiwa walikamatwa na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Chekereni na kufunguliwa mashitaka ya kulawiti jalada namba Teng/RB/570/2014, lakini siku moja baadaye waliachiwa huru, ndipo wana kijiji hao walipojikusanya na kuanzisha oparesheni ya kuwasaka na kufanikiwa kuwakamata hao.
Watuhumiwa hao walipohojiwa katika mkutano wa hadhara walikiri kujihusisha na matukio ya ulawiti wanaume wenzao.
Baada ya maelezo ya watuhumiwa hao, mwenyekiti huyo aliwakabidhi mikononi mwa jeshi la polisi Kituo Kikuu cha Arusha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema suala hilo bado lipo kwenye uchunguzi.
Posted