Imekaa poa sana! Miezi
kadhaa baada ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers
kufichua uchafu wa biashara haramu ya ngono kwenye Mtaa wa Mwanzo Mgumu,
Kata ya Mwembesongo, maeneo ya Msamvu mjini hapa, warembo wanaojiuza
eneo hilo wamekula kibano na malori yanayopaki mahali hapo yametimuliwa.
Baadhi ya machangu walionaswa wakijiuza.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, kiongozi wa mtaa huo, Said Omar Kamba
alisema: “Kwanza nayapongeza magazeti ya Global (Publishers) kupitia
kitengo chao cha OFM ambao walivamia Kambi ya ltingi (Msamvu) kwa
kushirikiana na polisi na kuwafuma wanawake waliokuwa wakifanya biashara
haramu ya kuuza miili na kutupa hovyo kondom ambazo watoto wa mtaani
kwetu walikuwa wakiziokota na kupuliza wakidhani ni mapulizo, jambo
ambalo ni hatari.
“Baada ya habari hiyo kuripotiwa na
magazeti ya Global, tumewatimua wanawake wanaojiuza baada ya kuketi
kikao cha Baraza Maalum la Kata ‘BMK’ na kukubaliana kwamba dawa yao ni
kuyaondoa malori eneo hili la ltingi.
Machangu hawa walinaswa wakiwa katika chumba kimoja.
“Uchunguzi wetu ulibaini kwamba madereva na ‘mataniboi’ huwanunua
wasichana hao na kufanya nao ngono kwenye malori na baadaye kutupa hovyo
kondom, kimsingi eneo hili ni ‘rizevu’ ya barabara ya Tanroads na
tumeshawasiliana nao juu ya uamuzi huo.”
Alipoulizwa malori hayo sasa yamehamishiwa wapi, kiongozi huyo
alisema: “Tumeyatengea eneo la Njia-Panda ya Tungi nje kidogo ya Mji wa
Morogoro.”