Aunt Ezekiel Akanusha Taarifa za Kujifungua
Baada ya kuzagaa taarifa za staa wa filamu nchini Aunt Ezekiel kujifungua, mwanahabari wa GPL ametia timu nyumbani kwa Aunt na kujiridhisha pasipo na shaka kuwa mrembo huyo bado yu mjamzito na taarifa za kujifungua si za kweli.
Mitandao mbalimbali ya kijamii imeripoti taarifa za Aunt kujifungua kuanzia jana huku mingine ikimpongeza na kuweka kipande cha video kinachomuonyesha mwigizaji huyo akiwa ammbeba mtoto mchanga.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Aunt Ezekiel jana aliweka kipande cha video akiwa amembeba mtoto mchanga bila kuandika chochote ambapo mashabiki wake walimiminika na kuanza kumpongeza wakijua tayari kajifungua.
Akiongea na mwanahabari wa GPL Aunt amesema kuwa , hicho ni kipande cha mojawapo ya filamu yake aliyocheza siku nyingi. Na taarifa zilizoenea mitandaoni kuwa kajifungua si za kweli.
Kwa upande wa pili kijana anaesemekana ndio alimpa ujauzito huo, Mosesi Iyobo ambae ni mcheza dansi wa mwanamziki Diamond alibandika mtandaoni picha ya mama akiwa amebeba katoto (itazame hapo juu) na kupeleka watu kumpa pongezi pia.
Posted