Home » Uncategories » HII MICHEPUKO SASA DUUH!! NJEMBA LABABWA MARA BAADA YA MKEWE KUFANYA MSAKO MKALI!!!
HII MICHEPUKO SASA DUUH!! NJEMBA LABABWA MARA BAADA YA MKEWE KUFANYA MSAKO MKALI!!!
Aibu iliyoje! Tukio la aina yake limetokea maeneo ya Diluxe jijini Mwanza baada ya mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Faudhia almaarufu mama Baraka kumfumania mumewe akisaliti ndoa yao mbichi. Kwa mujibu wa mama Baraka, amekuwa akimfuatilia mumewe kwa muda mrefu baada ya kutonywa na wambeya kuwa baba mtoto wake huyo amekuwa akichepuka na ‘kichenchede’ (mrembo) wa mjini. Siku ya tukio, hivi karibuni ilidaiwa kwamba mume huyo alirudi nyumbani mapema, akapumzika kidogo, majira ya saa sita mchana aliamka, akaoga na kupewa chakula kama kawaida kisha akamuaga mkewe kuwa anaenda ofisini kuna dharura imetokea ghafla.
Kwa mujibu wa mke huyo, jamaa alipotoka tu naye akachukua pikipiki ambayo ilikuwa tayari imeandaliwa na kuanza kumfuatilia kwa nyuma kila alipokuwa anaenda ambapo alienda katika baa mbalimbali za Villa Park Resort, Kibo na nyingine.
Ilisemekana kwamba, alipofika Diluxe Night Club, alipiga honi kisha akajitokeza kimwana mmoja na kuingia kwenye gari hilo wakaondoka, walipofika kwenye eneo la giza maeneo hayohayo ya Diluxe Night Club, gari lilisimama, wakashuka, wakahamia siti ya nyuma.
walifika maeneo hayo na kukuta timbwili la nguvu ndani ya gari huku mama mmoja aliyevaa kininja akimwadhibu msichana aliyekuwa nusu utupu na mumewe ndani ya gari.Wakati wa timbwili hilo, mchepuko alivaa suruali na kusahau kuvaa kufuli pakaendelea kuchimbika.
MAMA BARAKA AFUNGUKA
Akiwa eneo la tukio, mama Baraka alisema kuwa alikuwa na kazi kubwa ya kumfuatilia mumewe kwa siku nyingi lakini mumewe huyo alikuwa akipiga chenga.“Nilianza kumfuatilia mume wangu kwa muda mrefu sana baada ya kupata taarifa kuwa huwa ana tabia ya kufanya mapenzi kwenye gari na wanawake.“Nilishamuuliza zaidi ya mara tatu kutaka kujua kama kweli ana tabia hiyo lakini alinikatalia katakata.”
mwenye mme akiwa kasimama kwenye gari ya mumewe wakati wachepukaji wamo ndani ya gari
MUME ATAKA KUKATA MSHIKO.
Mume huyo alipoulizwa juu ya tabia hiyo alikataa katakata kuongea na kuwambia wadakuzi wetu kuwa hayo mambo anaomba yaishie hapohapo kisha kuzama kwenye waleti na kutoa fedha.
Hata hivyo, makamanda wetu walizikataa na kuendelea kufanya kazi yao kwa mujibu wa kiapo chao cha kutopokea hongo wala rushwa hivyo waliondoka eneo hilo wakimwacha mama Baraka akipambana na mumewe huku binti akiachiwa aende zake.
Posted